Serikali ya Zanzibar inajipanga kuweka miundombinu mizuri ya maeneo ya kufanyia mikutano, ili kutumia vyema fursa ya kuwa na utalii wa mikutano.

Kauli hiyo, imetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakati akizungumzia Miaka Mitatu ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane Zanzibar.

Amesema, “kinachotakiwa kufanyika hivi sasa ni kujipanga kuweka miundombinu mizuri maeneo ya kufanyia mikutano hiyo, lengo ni kuitumia fursa kwa Zanzibar kuwa na utalii wa Mikutano.”

Amesema, sekta binafsi zinatakiwa kuangalia uwezekano wa kuweka kumbi mbalimbali za mikutano. ili kuwezesha kufanyika kwa mikutano mingi, hali itakayochangia uwepo wa wageni na watalii wengi.

Michezo Serikali za Mitaa; Muleba wapokea Kombe, Medali
Waafrika ruksa kuingia Rwanda bila Visa - Kagame