Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema uvamizi wa Urusi nchini humo utamalizika tu kupitia diplomasia.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo Rais Zelensky amesema hayo wakati wa mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yakivunjika huku pande zote mbili zikilaumiana kwa kutolegeza misimamo.
Suala kuu linalokwamisha mazungumzo hayo ni iwapo Urusi inapaswa kuendelea kushikilia maeno iliyoteka wakati wa vita, ama kurudi kwenye mipaka yake inayotambulika kimataifa.
Wakati huo huo, Urusi inaonekana kufanya mashambulizi makubwa katika eneo la mwisho lililosalia linaloshikiliwa na Ukraine huko Luhansk.
Luhansk inaunda sehemu moja ya eneo kubwa la Donbas, ambalo Urusi imetangaza kuwa sasa ndilo lengo lake kuu nchini Ukraine.