Jeshi nchini Burkina Faso limetangaza vifo vya wanajeshi wake 11 kufuatia shambulio lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi kutoka katika vikosi vilivyopo mashariki mwa nchi hiyo.

Katika ripoti yake ya Mei 20, 2022 Jeshi hilo limesema idadi hiyo imeongezeka ikiwa ni vifo vipya baada ya awali kutangaza vifo saba vilivyotokana na shambulio la awali mapema hapo jana Mei 19, 2022.

“lilikuwa ni shambulio tata milio ya makombora iliyofuatiwa na moto wa moja kwa moja kwenye kambi ililenga kikosi cha kijeshi cha Madjoar katika jimbo la Kompienga eneo letu la mashariki,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema wanajeshi hao 11 waliopoteza maisha katika shambulio hilo walikuwa doria na wengine 20 kujeruhiwa na baadhi yao walitibiwa na watu wa huduma za afya nje ya eneo la jeshi.

“Hata hivyo ndege za jeshi ziliingilia kati na kuwazuia magaidi wasiopungua 15 waliokuwa wakijaribu kutoroka baada ya shambulio hilo ambao huenda wangeleta madhara zaidi,” ilisema taarifa ya jeshi.

Alhamisi Mei 19, 2022 watu waliokuwa na silaha walishambulia basi eneo la Seytenga jimbo la kaskazini la Séno nchini humo ambapo raia mmoja aliuawa na abiria wengime 12 kujeruhiwa kabla ya tukio la baadaye la wanajeshi saba kuuawa.

Jumamosi Mei 14, 2022 wasaidizi 40 wa jeshi na raia waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika mashambulizi matatu tofauti kwenye eneo hilo.

Burkina Faso hasa maeneo ya  kaskazini na mashariki yamekuwa yakishambuliwa na wanajihadi wa vuguvugu la al-Qaeda na Islamic State tangu mwaka 2015 ambalo limeua zaidi ya watu 2,000 na wengine milioni 1.8 kuyakimbia makazi yao.

Bahari yameza wahamiaji , maelfu wako njiani
Watu wawili mbaroni kwa kuazimisha silaha