Imeelezwa kuwa mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza vitamini A pekeyake hivyo unahitaji vykula ambavyo vitasaidia kutengeneza, ambapo vitamini hivyo ni mojawapo ya virutubishi muhimu katika kipindi chote cha maisha ya binadamu.
Afisa Lishe kutoka Taasisi ya chakula na lishe TFNC, Vumilia Lyatuu amesema vitamini A pamoja na mahitaji mengine huitajika mwilini sana kwakuwa na faida yingi mwiini ikiwepo ya kusaidia macho kuona vizuri.
Amesema faida nyingine ni kwamba husaidia katika ukuaji na maendeleo ya mimba na mtoto, na kuongeza kinga ya mwili dhidi ya maradhi mbalimbali.
Mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi, matunda yenye rangi ya manjano, mafuta ya mawese, karoti na viazi vitamu vyenye rangi ya njano ni miongoni mwa vyakula vyenye vitamini A nyingi zaidi.
pia vyakula vitokanavyo na wanyama kama maziwa ya wanyama, mtindi, siagi, jibini, nyama, samaki, maini, kiini cha yai navyo ni miongoni mwa vyakula vyenye vitamini A kwa wingi.
Baadhi ya madhara ya upunguvu wa vitamini A ni kutoona vizuri, mjamzito kujifungua kabla ya miezi tisa, na huweza kupelekea vifo kwa mama wajawazito.