Makamu wa rais nchini Zimbabwe, Kembo Mohadi ametangaza punguzo la bei za bidhaa na huduma muhimu ili kuwawezesha wananchi wa nchi hiyo kukabiliana kikamilifu na maambukizi ya virusi vya corona.
Akizungumza na wazalishaji viwandani na wauzaji rejareja wa bidhaa mbalimbali amesema taifa limekuwa likishuhudia ongezeko la bidhaa na huduma muhimu ambazo wananchi hawazimudu.
Pia uchunguzi uliofanywa na wizara ya viwanda na biashara nchini humo kati Februari na April 11umebaini kuwa bei za bidhaa zimepanda kwa asilimia 42.
Hata hivyo punguzo hilo la bei za bidhaa na huduma muhimu nchini humo limekubaliwa kwa pamoja kati ya serikali na wafanyabiashara.