Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameilalamikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kwa kuvunja kifungu cha sheria namba 13 ya mwaka 2017 kifungu 47(2) kinachowataka kufunga hesabu za pesa za kila mwaka.
Zitto amesema Takukuru ina miaka mitano haijakaguliwa na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na kila mwaka inapewa kiasi cha tsh bilioni 85 lakini mpaka sasa ni miaka mitano haijafunga hesabu wala kukaguliwa na CAG.
-
Video: Lissu amsubiri ndugai kwa hamu, Mangula arudishwa
-
Trump akanusha kutaka kumfukuza kazi mwendesha mashtaka
‘’Licha ya kupewa tshs 84 bilioni kila mwaka, Takukuru hawana mahesabu ( annual accounts ) na hawajakaguliwa na mkaguzi yeyote. Jeshi letu JWTZ lina kaguliwa na CAG na kuitwa mbele ya PAC Lakini Takukuru hata hesabu hawafungi.”amesema Zitto Kabwe.
Zitto ameeleza kuwa Takukuru ni taasisi nyeti inayotakiwa kuwajibikia nchi bila kuegemea upande wowote kwani amesema kwa sasa taasisi hiyo inafanya kazi ya kutumika kisiasa.
“TAKUKURU ni moja ya taasisi nyeti za uwajibikaji nchini Lakini inatumika kisiasa. inatumwa na wanasiasa wa CCM kufanya mambo yao’’
Hata hivyo Zitto ameeleza kuwa kukamatwa kwa Mwalimu Mukoba jana ni moja ya ushahidi wa kutumika kwa Takukuru kisiasa kwani Serikali ina lengo ya kudhibiti Chama cha Walimu nchini na kina Mukoba walionekana ni vikwazo.
‘’Sitaki kusema la Nehemia Mchechu wa NHC Lakini nina hakika ya dhati amekuwa fixed sababu ya chuki, visasi na roho mbaya. Takukuru wanatumika kwenye hayo’’. Amesema Zitto.
Kwa upande mwingine Zitto Kabwe ameitaka Takukuru kuacha kutumika kisiasa na kuionya kuwa isipokuwa makini huenda ikawa jumuiya ya nne la CCM.