Takukuru yautupa ushahidi wa video wa wabunge wa Chadema, Joshua Nassari na Godbless Lema ukiwaonyesha madiwani wa chama hicho waliohamia CCM wakihongwa rushwa.

Madai hayo yametupiliwa mbali kwa kile kilichodaiwa kuwa  wabunge hao waliharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.

Imeeleza wabunge hao waliingilia uchunguzi na kuuvuruga ila hawawezi kusema ni jambo gani walivuruga kwa sababu mambo mengine ni ya kiuchunguzi.

Hivyo Takukuru imeamua kutupilia mbali ushahidi huo wa video uliowasilishwa kwa flash na wabunge hao wa Chadema kwa kudai kuwa kuna kanuni za utoaji wa ushahidi, video kama zilivyo haziwezi kuwa ushahidi tosha.

‘’Ile ni taarifa na ushahidi ni tofauti’’ amesema Musa Msalaba ambaye ni msemaji wa Takukuru.

‘Ni kweli flash tulikabidhiwa lakini Nassari na wenzake kwa sababu walivuruga uchunguzi hatuwezi kuendelea kufanya siasa kwa sababu ya uchunguzi lazima uwe huru,;; amesema Msalaba.

Hata hivyo amesema kuwa kutokana na teknolojia kuwa kubwa zama hizi mtu anaweza kuzichezea na kutengeneza kitu kama hiko na kikaonekana kweli.

 

Heche: Serikali haijawahi kupambana na rushwa
Zitto aiwashia moto Takukuru