Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Ruyagwa Kabwe leo amefikishwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kujibu tuhuma zinazomkabili za kudharirisha Bunge kama alivyotakiwa na Spika, Job Ndugai.
Aidha, mara baada ya kufikishwa Dodoma kwaajili ya kujibu tuhuma hizo Zitto amekiri kuwa ni kweli alitoa kauli hiyo kwakuwa ni haki na uhuru wake wa kutoa maoni na alilenga kulinda hadhi ya bunge.
“Ni kweli nilitoa kauli hiyo kwa sababu ni haki yangu ya msingi kutoa maoni, na sikuwa na lengo baya kwani nililenga kulinda uhuru, hadhi na kulinda heshima ya bunge,”amesema Zitto Kabwe
Hata hivyo, ameongeza kuwa kama bunge litaendelea kupokea maelekezo kutoka Ikulu na kusimangwa na Serikali, basi litakuwa sio bunge tena bali litakuwa ni Tawi tu la Serikali na kamati hiyo itazidi kuita Watanzania wengi kwaajili ya kuwahoji.