Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amekamatwa na jeshi la polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) uliopo jijini Dar es Salaam akitokea Kigoma.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis ambapo amesema kuwa kiongozi huyo wa chama chake amekamatwa hivyo wanasheria wa chama hicho wanafuatilia kujua sababu ya kiongozi wa chama chao kukamatwa na jeshi la polisi.

“Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es salaam wakati akitoka Kigoma. Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake,”amesema Khamis

Hata hivyo, kulikuwepo na taarifa za Katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashililah kutoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo wa Kigoma Mjini na kutakiwa kumfikisha mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kauli ambazo amewahi kuzitoa juu ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai pamoja na Bunge lenyewe.

JPM awaweka mtegoni wawekezaji matapeli
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 21, 2017