Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa uchungu anaoupata baada ya kuunguliwa na nyumba yake umemfanya kuwafikilia wananchi wanaobomolewa nyumba zao bila fidia.
Ameyasema hayo kupitia ukurasa wake Facebook mara baada ya kuitazama nyumba yake ya kwanza iliyoteketea kwa moto mwishoni mwa wiki iliyopita huko Mwandiga mkoani Kigoma.
“Sikudhani kabisa kuwa naweza kuumizwa na kupata uchungu kwa tukio kama hili na ninajiuliza huu uchungu ni wa nini? Kumbe ni uchungu wa nyumba ya kwanza. Nawafikiria wananchi wenzangu wanaobomolewa nyumba zao bila fidia, na wengi ni nyumba zao za kwanza na pekee. Uchungu wao nausikia. Hasira zao nazihisi,”amesema Zitto
Amesema kuwa ameridhika kwa kile kilichotokea kwenye nyumba yake kuungua moto kwakuwa ni ajali ya kawaida na wala watu wasichukulie kwa muktadha wa matukio yanayoendelea nchini kwa sasa.
-
Mbunge Musukuma na wenzake wapandishwa kizimbani
-
Lissu ampa ujumbe mzito Zitto, ‘Tumeshinda’
-
JPM atuma salamu za rambirambi ajali ya Uganda
Hata hivyo, Nyumba ya Zitto Kabwe iliyoungua hivi karibuni huko Mwandiga Mkoani Kigoma inadaiwa kuwa ndiyo nyumba yake ya kwanza baada ya kupata ridhaa ya kuwa mbunge.