Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba SC Zoran Maki amefunguka kwa mara ya kwanza kilichosababisha kuondoka klabuni hapo, mwezi mmoja baada ya kuanza kazi.
Zoran Maki aliondoka Simba SC, Septemba 2022 akiiongoza timu hiyo katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans.
Akihojiwa nchini Misri anakofanya kazi akiwa na klabu ya Al Ittihad, Kocha huyo kutoka nchini Serbia amesema alilazimika kuondoka Simba SC, kufuatia ofa nzuri aliyoipata.
Maki amesema mbali na ofa hiyo, pia ukubwa wa soka la la nchini Misri ulimvutia kukubali kirahisi kwa kuvunja mkataba wake na Simba SC.
“Najua Ukubwa wa soka la Misri na ndiyo maana ofa ilipotoka kwa Al Ittihad, mara moja nilisema ndiyo na kuikataa Simba SC na kuja hapa.” amesema Zoran Maki
Kabla kutua Simba SC kocha Zoran Maki aliwahi kuvinoa vikosi vya klabu za Primeiro de Agosto (2017–2019), Wydad AC (2019–2020), Al-Hilal Club (2020–2021) , CR Belouizdad (2021) na Al-Tai (2021) .