Kiungo Mshambuliaji Kutoka Burkina Burkina Faso Stephanie Aziz ameitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya nchi hiyo, kwa ajili mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Kocha Mkuu wa Burkina Faso Hubert Velud, amemtaja kiungo huyo katika kikosi chake, baada ya kufuatilia mwenendo wake akiwa Young Africans, ambayo ilimsajili mwanzoni mwa msimu huu, akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Burkina Faso itacheza michezo miwili ya kuwania kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Togo mwishoni mwa mwezi huu, nyumbani na ugenini.

Mchezo wa Machi 24 Burkina Faso itakuwa nyumbani ikiikaribisha Togo katika Uwanja wa du 4-Août mjini Ouagadougou, kisha itacheza mchezo wa pili dhidi ya Togo ugenini mjini Lome katika Uwanja wa de Kégué.

Hatimaye Godbless Lema awasili nchini
Chalamila: Viwanja visivyoendelezwa vifutwe