Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amemuagiza Afisa Mipango, na Kamishna Msaidizi wa Halmashauri ya Bukoba kubaini viwanja visivyoendelezwa vilivyopo katikati ya manispaa hiyo, ili vifutwe na kukabidhiwa kwa watu wengine kwa sharti la kuviendeleza na kuukuza mji wa Bukoba.

Chalamila ametoa kauli hiyo katika kikao cha kamati ya ushahuri mkoa (RCC), cha kujadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2023/2024, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila.

Amesema “nimeshamwambia Mkuu wa mipango miji wa Bukoba wakisaidiana na kamishna watafute viwanja ambavyo tangu miaka ya 90 haviendelezwi ambavyo vimeendelea kuufanya mjiwetu uonekane ni magofu na kuonekana ni mji ambao hauendelei.”

Chalamila ameongeza kuwa, “viwanja hivyo tuvipeleke mlamlaka ya Rais kuvifuta ili waweze kumilikishwa wengine kwa masharti ya kuendeleza na kubadilisha mji wa Bukoba.”

Aziz Ki aitwa timu ya taifa Burkina Faso
Young Africans yahamia Chamazi