Msanii mkongwe kwenye kiwanda cha Bongo Flava, Said Juma Hassan maarufu kwa jina la Chege Chigunda na mchumba wake anayejulikana kwa jina la Zahra wamefanikiwa kupata mtoto wa kike.

Mkali huyo anaye tamba na wimbo wake wa ”Kaitaba” akiwa amemshirikisha Saida Karoli ameweka wazi furaha yake hiyo ya kupata mtoto kupitia akaunti yake ya mtandaoo wa instagram baada ya kuweka picha akiwa na mama wa mtoto huyo aliye pewa jina la Jadah.
Kufuatia picha hiyo wasanii wengi wamempongeza kwa kumtakia furaha na malezi bora ya mwanae.
Hata hivyo Chege amemfungulia mtoto wake akaunti ya instagram ambayo mpaka sasa ina wafuasi 2,342.
Moja ya maneno aliyoandika Chege kwenye ukurasa wake mara baada ya kufungua akaunti hiyo ameandika hivi.
”Kweli Jadah_chege umekuja na Baraka zako naona kuna page zaidi ya kumi za j but siyo zenyewe Acount Original ya jadah ni @Jadah_Chege.

 

 

 

Naibu Katibu Mkuu Bavicha ajiuzulu
Azam FC yawashusha mabingwa watetezi

Comments

comments