Marais watano wa zamani nchini Marekani wamekusanyika katika tamasha la kuchangisha fedha za kuwasaidia waathirika wa janga la kimbunga ambacho kiliyakumba maeneo kadha ya Marekani.
Rais Barack Obama, George W Bush, Bill Clinton, George HW Bush na Jimmy Carter wote walikutana Texas hapo jana kwa lengo la kuwasaidia wale walikumbwa na janga la vimbunga Irma na Maria.
Marais hao wamefanikiwa kuchangisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 31 hadi sasa mchango ambao utasaidia jamii za Florida, Puerto Rico na visiwa vya Marekani vya Virgin vilivyopigwa na kibunga.
-
Korea Kaskazini yaapa kutositisha mpango wa silaha za nyuklia
-
Trump kuamuru siri ya mauaji ya ‘Rais Kennedy’ kuwekwa hadharani
-
Uteuzi wa Mugabe kuwa balozi wa ‘WHO’ waibua maswali
Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump hakuhudhuria, lakini alituma ujumbe kabla na kuwapongeza marais hao kwa kazi yao nzuri.
Tamasha hilo wasanii mbali mbali akiwemo akiwemo Lady Gaga TrumpLyle Lovett, Robert Earl Keen, Sam Moore na Yolanda Adams walitumbuiza.