Mjumbe wa Korea Kaskazini Choe Son Hui amesema kuwa Marekani italazimika kukubali kuishi na Korea Kaskazini yenye silaha za kinyuklia kwa kuwa nchi hiyo haina mpango wa kusitisha mpango wake wa silaha hizo.

Choe Son Hui amesema kuwa kuendelea kuwa na silaha za nyuklia ndio njia pekee ya kuwa na amani ya kudumu katika rasi ya Korea.

Akizungumza katika kongamano la kuzuia kuenea kwa silaha za kinyuklia mjini Moscow, bi Choe alisisitiza kwamba silaha za kinyuklia ni swala la ”maisha na kifo” kwa taifa hilo.

Mkurugenzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani Mike Pompeo alionya kwamba Korea Kaskazini inaweza kuishambulia Marekani na kombora la kinyuklia katika kipindi cha miezi michache ijayo jambo ambalo Korea Kaskazini imethibitisha kuwa na uwezo nalo.

Pompeo amesisitiza kuwa Washington bado inataka kutatua swala hilo kidiplomasia na vikwazo lakini ikasema inaweza kulazimika kutumia nguvu iwapo Korea Kaskazini itaaendelea na mipango yake ya nyuklia.

Tangu Korea Kaskazini ilipoanza kufanyia majaribio makombora yake mwaka huu, vikwazo dhidi ya taifa hilo vimeongezeka lakini Choe Son Hui anasema vikwazo hivyo ni hatua ya uchokozi na vita.

 

 

Video: Zitto Kabwe amvaa Prof. Kabudi kuhusu makinikia
Uteuzi wa Mugabe kuwa balozi wa 'WHO' waibua maswali