Mashindano maarufu ya Big Brother Africa ambayo yaliwaweka vijana wa Kiafrika kutoka nchi mbalimbali kwenye jumba moja kwa takribani siku 100 yameahirishwa.

M-Net imetoa taarifa rasmi kuhusu kuahirishwa kwa mashindano hayo ikieleza kuwa hivi sasa waandaaji wanafanya tathmini ya mashinano hayo.

“Wakati huu, timu iko bize ikifanya tathmini ya mkakati na muelekeo wa Big Brother Africa. Mnahakikishiwa kuwa itakaporudi itakuwa kubwa zaidi na bora zaidi,” taarifa ya M-Net inasomeka.

Huenda shindano hilo likarejea kwa nguvu kubwa zaidi na kitita kinene kitakachowaneemesha washindi.

Hadi sasa, taji la shindano hilo linashikiliwa na Idris Sultan, Mtanzania aliyenyakua kitita cha $300,000.

Familia ya Marehemu Kabwe yakananusha kutoishirikisha Serikali Mazishi
Ulevi wa Kitwanga ulivyowanyima Ukawa ‘pointi 3 muhimu’

Comments

comments