Mabingwa wa soka Barani Ulaya, Ureno walipokea kichapo cha kushangaza kutoka timu ya taifa ya Uholanzi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezewa mjini Geneva, Uswizi.

Winga wa zamani wa Manchester United, Memphis Depay na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Ryan Babel waliongoza mashambulizi kwa kuichakaza Ureno gori 3- 0.

Aidha, katika mchezo huo, Mchezaji wa Ureno, Joao Cancelo alipewa kadi nyekundu dakika ya 61 baada ya kupata kadi mbili za njano.

Hata hivyo, katika mchezo huo, Cristian Ronaldo alishindwa kufurukuta mara baada ya kudhibitiwa na mabeki wa timu ya taifa ya Uholanzi.

 

Arsenal yamuongezea mkataba kiungo Mohamed Elneny.
Wizi wa mtandaoni wawatia mbaroni 3

Comments

comments