Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz na Faustina Charles maarufu kama Nandy, mapema leo hii wamewasili katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kufuatia kusambaa mitandaoni kwa video zao wakiwa faragha zilizodaiwa kukosa maadili.

Hata hivyo hivi karibuni Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Harrison Mwakyembe aliagiza kukamatwa kwa wasanii hao kwa ajili ya upelelezi kisha kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili ya kukiuka maadili na kusambaza video hizo chafu.

Tazama Video hapa chini ikionesha Diamond na Nandy wakiwasili TCRA.

Siwa ya Bunge la Nigeria yapatikana baada ya kuibiwa
Serikali kujenga makumbusho ya marais wastaafu