Msanii wa muziki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wasafi Media, Diamond Platinumz amesema kuwa hapendi tabia ya baadhi ya wasanii kutaka kutoa pesa ili kazi zao zichezwe kupitia Wasafi TV na Wasafi Radio.

Diamond ametoa onyo kwa wasanii wanaojaribu kutoa hongo ili kupata nafasi hiyo kuwa endapo atawabaini atazifungia kazi zao kuchezwa kwenye vituo hivyo.

Hivyo, amewataka wasanii kutumia Wasafi TV na Wasafi Radio bure kurusha kazi zao kwani lengo kubwa la kuanzishwa kwa kampuni hiyo ni kuhakikisha kazi za wasanii hapa nchini zinafika mbali na  kila msanii anayefanya kazi nzuri apate nafasi stahiki.

Diamond Platinumz aliyasema hayo jana katika mkutano kati ya wasanii wa filamu na muziki wa mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

Msikilize hapa chini, ambapo mbali na hayo pia ametoa ushauri kwa Mkuu wa Mkoa utakaowasaidia wasanii wenzake katika kufikisha kazi zao za sanaa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Video: Masanja amuomba Makonda kuwanasua wasanii kwenye upangaji
Lissu auchokoza mkeka wa Ndugai, ‘sijawahi kulipwa senti’

Comments

comments