Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Swabri Mohammed maarufu kama Redsan amemshambulia mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania, Sappy ambaye anafanya kazi zake  jijini Nairobi.

Sappy amesema kuwa walikuwa studio, mara msanii huyo aliingia na kuanza kumhoji kwanini hakutokea kwenye uzinduzi wa albamu yake iliyozinduliwa wikiendi iliyopita, Septemba 15 na kwanini hakupokea simu yake kisha msanii huyo akaanza kumrushia ngumi na maneno machafu mtayarishaji huyo.

Hata hivyo kwa mujibu wa ”tweets” mbalimbali inasemekana kuwa Sappy hakulipwa pesa yake mara baada ya kumtayarishia albam mwanamuziki huyo.

Aidha, Redsan ameahidi  kumtafuta promota aliyemtelekeza kwenye mataa msanii wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage kwani alikuwa ni moja ya wasanii wakubwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa album yake.

Muonekano wa Sappy mara baada ya kupigwa na msanii huyo, Redsan.

CAF yamsafisha Jerry Yekeh
Video: Haya ndiyo maisha halisi ya Hamissa? 'Madam Hero'

Comments

comments