Wenyeji wa Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) 2021, Young Africans wameanza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Nyasa Big Bullet kutoka nchini Malawi.

Young Africans ilitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Mshambuliaji mzawa Waziri Junior dakika ya 8, kabla ya Big Bullet hawajasawazisha kwa mkwaju wa penati iliopigwa na Chiupeko Msowoya dakika ya 30, baada ya beki Abdallah Shaibu Ninja kumchezea hivyo Babatunde katika eneo la hatari.

Hata hivyo Young Africans walimaliza mchezo wakiwa pungufu, kufuatia Mlinda Lango Ramadhan Kabwili kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na mchezo usio wa kiungwa aliomchezea mchezaji wa Big Bullet.

Mchezo wa pili wa Kundi A utachezwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Express ya Uganda dhidi ya Atlabara kutoka Sudan Kusini.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 2, 2021
Mayele atambulishwa Young Africans