Takriban watu 12 akiwemo Waziri wa afya na Naibu Mkuu wa Wilaya wamefariki, katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye Makao Makuu ya Serikali ya mtaa wa Beledweyne, uliopo mji Mkuu wa eneo la Hiran nchini Somalia.
Mamlaka za usalama nchini humo, inasema katika tukio hilo watu 10 walijeruhiwa na majengo kuharibiwa katika milipuko hiyo huku Polisi wakidai Waziri wa afya wa jimbo hilo na Naibu Mkuu wa Wilaya ni miongoni mwa waliofariki.
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu, al-Shabab, limedai kuhusika na tukio hilo baada ya Hiran kuwa katikati ya uhamasishaji wa hivi karibuni dhidi ya waasi, wenye uhusiano na al-Qaeda.
Inaaminika kuwa, milipuko hiyo ya kujitoa mhanga inaweza kuwa ni ya kulipiza kisasi mauaji ya mwishoni mwa wiki ya Kiongozi Mkuu wa al-Shabab katika shambulio la ndege isiyo na rubani.
Hata hivyo, Mamlaka zilitangaza saa chache kwamba Abdullahi Nadir, ambaye alikuwa na fadhila ya $3m, aliuawa katika operesheni ya pamoja ya Jeshi la Taifa la Somalia na vikosi vya washirika wa kimataifa.
Hata hivyo, bado hijabainika ni nani aliyesaidia katika operesheni hiyo, lakini jeshi la Somalia linaungwa mkono na wanajeshi kutoka Marekani na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na hivi majuzi Somalia ilitangaza ‘vita kamili’ dhidi ya al-Shabab, ambayo inadhibiti maeneo mengi ya nchi hiyo ya kusini na katikati.