Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amesema Serikali inatekeleza mpango mkakati ambao unafanyiwa mapitio kila mwaka, ili kuona mapungufu kwa lengo la kurekebisha makosa na kukuza ufaulu kwa shule.
Telack ameyasema hayo hii leo Februari 21, 2023 katika ziara ya Waziri Mkuu ya kutembelea shule za Sekondari za Lucas Malia na Mary Majaliwa za Ruangwa na kuongeza kuwa mpango huo umesaidia kupunguza daraja sifuri kwa asilimia 40 na daraja la nne kwa zaidi ya asilimia 45 na kuongeza kuwa.
Amesema, “asilimia zaidi ya 50 ya waliomaliza mwaka jana wataenda kidato cha tano na tunauhakika mtoto aliyemalia kidato cha sita mkoani Lindi anakwenda chuo kikuu.”
Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu mama Mary Majaliwa amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii na wasijihusishe na makundi maovu na badala yake waweke malengo katika masomo yao ili waweze kutimiza ndoto zao kielimu.