Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, Walid bin Talal Al Saudi, juu uendelezaji wa mfuko wa Utamaduni na Sanaa.

Yakubu amefanya mazingumzo hayo na Mwna mfalme hii leo Februari 21, 2023 katika jengo la Kingdom Tower lililopo jijini Riyadh.

Katika mazungumzo yao, Al Waleed ameahidi kusaidia fedha kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa pamoja na kutoa misaada mingine kwenye tasnia ya Sanaa kupitia taasisi yake ya Al Waleed Philanthropies.

Katika safari hiyo, katibu Mkuu Yakubu aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini.

Mradi wa makazi wakaribisha wawekezaji Visiwani
Turekebishe makosa kukuza ufaulu: RC Telack