Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuungana na wananchi katika kuimarisha miundomibu ya elimu ili kuhakikisha watoto Wakitanzania wanapata elimu bora na kutimiza ndoto zao.

Majaliwa ameyasema hayo hii leo Februari 21, 2023 alipotembelea shule za Sekondari za Lucas Malia na Mary Majaliwa, zilizopo Ruangwa Mkoani Lindi na kuongeza Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wanapata elimu bora kuanzia ngazi ya elimu msingi hadi chuo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibeba tofali.

Amesema, pamoja na Rais Dkt. Samia kuweka mkazo katika kuipa hadhi sekta ya elimu, pia amewekeza kwenye elimu ya mtoto wa kike kwa kuweka sheria zitakazo muwezesha mtoto wa kike kutimiza ndoto zake

“Pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia anasimamia ubora wa elimu kwa watoto wote ikiwemo wakiume, watoto wetu wa kike tumewawekea mikakati ikiwemo sheria kali kwa wanaotaka kumkwamisha na sisi tunazisimamia ili aanze darasa ya awali mpaka atakapomaliza akiwa salama.”

Turekebishe makosa kukuza ufaulu: RC Telack
Waziri kundo ataka uhabarishaji shughuli za kimaendeleo