Abel Paul, Jeshi la Polisi – Arusha.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani wamesema watandelea Kusimamia Usalama wa vyombo vya moto, kufanya kaguzi za mara kwa mara na kutoa elimu kwa madereva, ili kumaliza ajali nchini.
Aidha, wamewataka pia mawakala wa mabasi kuandika taarifa kikamilifu zs wasafiri, ili kuwapa haki abiria kipindi inapotokea suala la malipo ama ajali.
Hayo yamesemwa Mapema leo Disemba 24, 2023 katika kituo kikuu cha mabasi Jijini Arusha na Mkurugenzi wa LATRA, Johansen Kahatano katika muendelezo wa ukaguzi wa vyombo vya moto na kufuatilia huduma za usafirishaji, ili kubaini changamoto zilizopo na nakuzifanyia kazi kwa wakati.
Ajali: Basi lagongana na Lori, wawili wafariki
Amesema, katika ukaguzi huo wameangalia nauli zinazolipwa kama ni nauli halali zillizotolewa na serikali mapema mwezi huu huku akiwapongeza watoa huduma kwa kujipanga vyema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo wanaendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
Mkurungenzi huyo Pia amesema kuna changamoto ambazo ni uandishi wa taarifa za abiria ambazo ni muhimu katika matumizi ya malipo ya kifedha ambapo amewataka mawakala kurekebisha mara moja changamoto hiyo.
Aidha Kahatano amesisistiza kuwa mawakala kote nchini wanapaswa kufuata sheria zilizopo huku akiwataka kuandika taarifa kamili za abiri ambazo zipo kwa mujibu wa sheria nataratibu za mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA,Pia amewataka mawakala hao kuandika vyema utambulisho wa mizigo ya abiri ili kuondoa changamoto ya upotevu wa mizigo ya abiria.
Nao baadhi ya abiria wanaotumia vyombo hivyo Kwenda maeneo tofauti tofauti ya nchi na nje ya nchi wasema ni vyema abiria wakatekeleza wajibu wao pindi wanaponda magari hayo kufunga mikanda ili iwasadie huku wakitaka madereva nao kufuata sheria za usalama barabarani zilizopo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Madereva Arusha – Moshi, Joseph Mwacha amesema madereva wa Mkoa huo wamekubaliana kufanya kazi hiyo kwa uadilifu, ili kuondokana ajali.