Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – FARDC, vimetoa onyo kwa kituo cha televisheni cha Nyota cha mwanasiasa wa upinzani Moïse Katumbi na vyombo vingine vya habari kwa taarifa ambazo zinadaiwa kutaka kuvuruga, kuvunja moyo na kuligawanya jeshi kupitia video, iliyosambazwa na Radio Okapi hapo jana Desemba 24, 2023.
Kwa mujibu wa Msemaji wa FARDC, Meja Jenerali Sylvain Ekenge Bomusa amesema Jeshi la Kongo litachukua hatua zinazohitajika kutekeleza sheria inavyoelekeza ikiwa hali hiyo itaendelea.
Amesema, “Televisheni ya Nyota na baadhi ya vyombo vya habari vinavyompa nafasi adui vimekuwa vikitangaza habari zilizotengenezwa na kituo hiki ili kuliyumbisha, kuvunja moyo na kuligawanya jeshi.”
Kufuatia hatua hiyo, Meja Jenerali Ekenge ameviomba vyombo hivyo vya Habari kujiepusha na utiaji wa sumu ya uchonganishi kwa wanajeshi na kuhusisha Vikosi vya FARDC kwa malengo ya kisiasa.