Shamrashamra za Krismasi zinaendelea kote duniani Jumatatu ya leo Desemba 25, 2023 siku ambayo Wakiristo wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo.

Wakiristo hutumia tarehe kama ya leo kwenda Kanisani na baadaye kusherehekea pamoja nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi.

Kihistoria, mwaka 274 M, kikomo cha jua kiliangukia Desemba 25, ambapo Mfalme wa Roma aitwaye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama (Natalis Solis Invicti) yaani Sherehe ya Kuzaliwa Jua Lisiloshindikana’.

Baadaye mwaka 320 M, Papa Julius I, aliitangaza Desemba 25, kuwa tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristo na mwaka 325 M, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini haikutiliwa maanani.

Mtakatifu Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa dhehebu la Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe isiyohamishika kwa tarehe 25 Desemba.

Hata hivyo, tunaona kwamba sio Biblia wala Yesu na wafuasi wake waliosema kitu kuhusu sherehe za Krismasi, wote walinyamaza na hata maandiko pia hayakuelekeza jambo kuhusu sherehe hizi, ingawa Mapagani wa Kirumi wao walisherehekea Desemba 25 kama ni ya kuzaliwa kwa ‘mungu’ wao wa nuru, aitwaye Mithra.

Kuna menginya kujifunza katika sikukuu hii lakini itoshe kusema HERI YA NOELI na ikumbukwe kila mwaka tarehe kama hii Mataifa husisitizwa juu ya upendo na kumcha MUNGU kupitia mwana wake YESU KRISTO.

 

Taasisi za Dini zipambanie ufundi, ujasiriamali - Kinana
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 25, 2023