Jenerali wa vikosi vya Jeshi Nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan ameapa kuendeleza vita kati ya jeshi la wanamgambo wa RSF, huku akizikataa juhudi za hivi karibuni za upatanisho wa kumaliza mzozo, kitendo ambacho kimetafsiriwa kuwa anataka vifo zaidi.
Burhan amesema waasi hao wamefanya uhalifu wa kivita na dhidi ya ubinaadamu huko Darfur Mashariki na maeneo mengi nchini Sudan na kudai kuwa hatakubali kupatanishwa na wala hakutakuwa na makubaliano.
Kwa upande wake, Kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo yeye alikubali kusitisha mapigano, kufuatia pendekezo la makundi ya kiraia.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mapigano ya Sudan yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 12,000 huku wengine zaidi ya milioni 7 wakilazimika kuyakimbia makazi yao.