Kampuni ya Uendelezaji wa Joto Ardhi Tanzania (TGDC) imetakiwa kuonesha Matokeo Chanya kwa kuzalisha Umeme kwa kutumia Rasilimali ya Jotoardhi ili kuunga Mkono Mpango wa Serikali wa kuwa na Nishati Safi na Endelevu.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati wa kikao na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo pamoja na Menejimenti ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukutana na baadhi ya Taasisi na Kampuni zilizo chini ya Wizara ya Nishati kwa lengo la kuona Utendaji kazi wa Taasisi hizo Tarehe 8 Januari 2024, Jijini Dar Es Salaam.

Ameitaka TGDC kuwa wabunifu na kutumia uwezo wao kuhakikisha inaanza kuzalisha umeme kwa kutumia Rasilimali ya Jotordhi kwa kuwa tayari baadhi ya maandalizi yameshafanyika katika maeneo ya vipaumbele.

“Nchi na Watanzania wanataka kuona umeme unaozalishwa kutokana na Jotoardhi,TGDC ni wakati wenu sasa kuonyesha uwezo wenu wa kuleta matokeo Chanya kwa Taifa, tumieni Ubunifu na Uwezo wenu wote kuhakikisha kile mlichokikusudia kinafanikiwa,” alisema Kapinga.

Kwa U

upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, amewaeleza TGDC kuwa ofisi yake iko wazi kupokea changamoto zinazowakabili, ili kuwasaidia na kuzitatua pale watakapoona wanakwama katika kutekeleza majukumu yako.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TGDC Prof. Shubi Kaijage na Meneja Mkuu wa TGDC, Mathew Mwangomba wamemuakikishia Naibu Waziri kuwa watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanazalisha umeme wa Jotoardhi haraka.

Kampuni hiyo, ina miradi mitano ya kipaumbele ukiwemo wa Ziwa Ngozi unaotajiwa kuzalisha Megawati 70 lakini kwa kuanzia wataanza na Megawati 30, Kiejo- Mbaka wa Mkoani Mbeya Megawati 60, Songwe Mkoani Songwe Megawati 5 hadi 38, Luhoi Mkoani Pwani Megawati 5 na Natroni Mkoani Arusha, Megawati 60.

Jamii ishiriki miradi ya ulinzi, usalama - Polisi
Mahundi amkalia kooni Mkandarasi Miradi ya Maji Lushoto