Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ruhembe iliyopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wametakiwa kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa taarifa pindi wanapoona dalili za vitendo vya Ukatili
Hayo yamesemwa hii leo Januari 9, 2023 na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi na Polisi Kata wa Kata ya Ruhembe, Flora Shayo wakati alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kutoa elimu juu ya ukatili.
Aidha, aliwafundisha Wasichana wa shule hiyo kuwa na msimamo na kuepuka vishawishi, huku akiwataka Wavulana kutojiingiza kwenye makundi ya watu wasio waadilifu kama wanaotumia madawa ya kuelevya na michezo ya kamari.
Mkaguzi Shayo aliunda Klabu ya wanafunzi ya Kupinga Ukatili yenye wanafunzi 15 na Mwalimu mmoja ambaye ni mlezi, huku Walimu wa Shule hiyo wakisema elimu hiyo ni msaada katika kubadilisha tabia za watoto.