Idara ya Polisi Kwale Nchini Kenya, imeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la visa vya watu kujitoa uhai katika hali tatanishi.

Idara hiyo imesema takriban visa vitatu vinaripotiwa kwa wiki vya watu kujinyonga  hadi kufa, kujiuwa kwa kutumia dawa ama sumu .

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kwale, Steven Ng’etich, amewataka wakazi wa maeneo hayo kutafuta huduma za ushauri nasaha, ili kukabiliana na matatizo ya msongo wa mawazo yanayowakumba.

Wakati hayo yakijiri, Mwili wa Mwanamke mmoja (67), umepatikana ukiwa na majeraha mabaya kichakani katika kijiji cha Bengo, kilichopo Lungalunga Kaunti hiyo ya Kwale.

Polisi wamesema Mwanamke huyo aliuawa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na  mwili huo ulikutwa na majeraha kichwani, shingoni na mkono wake wa kushoto ukikatwa kabisa.

DC Twange atangaza msako wa nyumba kwa nyumba
Mchengerwa amkabidhi Mhagama Mil. 20