Vijana wametakiwa kushiriki kufanya mazoezi sambamba na kutumia muda mwingi kujisomea kwa bidii na kufanya kazi, ili kujiepusha na vijiwe vya mazungumzo ambavyo baadhi ni chimbuko la uhalifu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Amina Haji Sipe katika uwanja wa Masipa shehia ya Pandani.

Alisema, uhalifu ni zao la jamii kwani hakuna mtu anaezaliwa nao, bali anaathiriwa na malezi, mazingira yaliyomzunguka na wakati mwingine aina ya marafiki alionao.

Amina aliongeza kuwa, Vijana wanaweza kujinasua na changamoto za mtaani kwa kutumia muda mwingi kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii au kwenda shule kujisomea na kujiepusha kukaa muda mrefu katika vijiwe.

Young Africans yatuma salamu Algeria
Makala: Mtafiti atafitiwa kwa mbio za Matunda