Jumla ya Wanafunzi 20 wa Shule ya Msingi Ifungila iliyopo kata ya Usangule Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, wamepatiwa vifaa mbalimbali vya shule ambavyo ni uniform, madaftari na kalamu, ili kuweza kumudu vyema masomo yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wanafunzi hao kurudi katika muhula mpya wa msomo shuleni bila vifaa vipya, wakidai walezi wao wameshindwa kuwanunulia kutokana na hali duni ya maisha.

Akiongea na Walimu na Wanafunzi wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Michael Rasha ambaye ni Polisi Kata wa Kata hiyo amesema, Kitendo cha Wanafunzi hao kurudi shule wakiwa na vifaa vya mwaka jana kimemgusa jambo ambalo limepelekea kuchukua maamuzi ya kuwanulia na kuwapelekea.

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Henry Mwangake anayehudumia Kata jirani na Usangule amewataka Wanafunzi hao kutumia fursa hiyo kusoma kwa bidii, ili waje kuwa msaada kwa familia zao.

Polisi Kata hao, pia walitumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa Wanafunzi namna ya kujilinda na vitendo vya Ukatili, maeneo ha kutoa taarifa pamoja kulindana wao kwa wao na kuwafundishwa miradi ya Polisi Jamii, ikiwemo Usalama wangu kwanza, Familia yangu haina muhalifu na kauli mbiu ya Polisi Jamii.

Kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo,  Mwalimu Ally Makambi Mohamed ametoa shukran za dhati kwa Askari hao na kuitaka Jamii kuiga mfano huo kwani kuna wanafunzi wengi ambao wanauhitaji wa vifaa vya shule katika shule hiyo.

Kocha msaidizi Taifa Stars matumaini kibao
Idadi Wanawake wanaomiliki ardhi Nchini yaongezeka