Lydia Mollel – Morogoro.

Ukatili wa kijinsia, umekuwa ni wimbo unaoimbwa na wengi kwa upande wa Wanawake na Watoto, licha ya kwamba kwa wanaume sauti hiyo ni changamoto kutokana na uhafifu katika kujitokeza na kuelezea changamoto wanazopitia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa pili ya WomenTogether Mkoani Morogoro, Mkuu Wa Dawati la  Jinsia Mkoa wa Morogoro  ASP Dkt. Mwanaidi Lwena amesema watu wengi hudhani wanaume wamesahaulika katika mapambano dhiti ya Ukatili wa Kijinsia lakini sivyo, kwani baadhi yao wanaona aibu kujitokeza na kueleza kile wanachokipitia.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Morogoro, Mkaguzi Pendo Meshurie amewataka Wananchi kujitokeza na kutoa taarifa zozote za ukatili kwani Dawati la Jisia ni sehemu salama

Naye Mkaguzi Paula Mhina, amesema Ofisi ya Polisi Jamii Mkoa wa Morogoro kupitia Dawati la jinsia, inashughulika na mapambano dhidi ya ukatili kwa kuanzisha miradi mbalimbali itakayowasaidia wananchi kupata elimu sahihi juu ya ukatili wa kijinsia.

‘Kuwa Shujaa Pinga Ukatili’ ndio Kauli Mbiu ya taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama Women Together ambao kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, watapaza sauti kupinga ukatili pamoja na kutoa elimu kwa jamii.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 17, 2024
Mchungaji ampika mboga Muumini wake ili asichepuke