Wakati wa utawala wa ubelgiji nchini DRC zamani Zaire, watu wa Taifa hilo walitumikishwa katika njia mbalimbali ikiwemo Kilimo katika mashamba ya Mpira huko Wilayani Nsongo, wakiwa na kiwango maalumu cha kufanikisha kazi za kila siku na endapo wasingefikia lengo, basi ilitolewa adhabu kwa muhusika.
Katika utaratibu huu, kulitokea tukio la Karne ya 20 (ilikuwa mwaka 1904), ambapo Mtu mmoja Mkulima, Mfanyakazi wa Kikoloni aliyefahamika kwa jina la Nsala Di Wala, alishindwa kumaliza robo ya kazi yake ya kuvuna Mpira kama Mkoloni alivyotaka, hali iliyopelekea bintiye kupoteza viungo vya mwili vilivyokatwa akiwa hai.
Binti huku Baali Nsala (5), baada ya baba yake kutofikia lengo la Mkoloni la kuvuna zao hilo la Mpira alikatwa mikono na Walinzi wa Mkoloni, kisha aliuliwa kinyama na haikutosha pia wakamuua mke wa Nsala kama adhabu ya kushindwa kufikia sehemu ya kazi aliyopangiwa, kwa siku husika.
Hata hivyo, hayo yote hayakutosha kwani waliona bado Nsala hajapata maumivu hivyo Walinzi hao wa Mkoloni walichukua mwili wa Mtoto wake Baali na Mama yake (Mke wa Nsala) na kuwafanya kitoweo kwa kuwakata vipande kisha kuwachemsha na kula nyama zao na mabaki wakapelekea Nsala mwenyewe.
Nsala Di Wala, alikuwa ni mtumwa kutoka nchi ya Zaire (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC), wakati huo ikitawaliwa na Ubelgiji chini ya Mfalme Leopod ambaye aliheshimishwa kwa mji mkuu wa nchi hiyo kupewa jina la Leopoldville kabla June 30, 1966 kubadilishwa na kuwa Kinshasa.
Pamoja na ukatili huo aliofanyiwa lakini hakuwa na la kufanya na alinyamaza kimya akiangalia mabaki ya ushahidi wa viungo vya Mwanaye na Mkewe bila kusema kitu hali ambayo aliionesha toka awali kwa kutosema chochote wakati mwanaye akikatwa, kuuliwa na hata mkewe kutolewa uhai na kuwashangaza Wakoloni hao.
Nadhani waweza vaa viatu vya mtumwa huyu wa Wilaya ya Nsongo (Nsala Di Wala), kujua ni hali gani alipitia wakati wa tukio hilo kukaa chini kama navyoonekana pichani akiangalia mabaki ya viganja vya mikono ya mwanaye na Mkewe, kisha pima aina ya maumivu unayopitia na angalia gumu ulilonalo linalokupa maumivu halafu chukua hatua ya kulipotezea kama ni dogo kwa hili la Nsala.
Inaelezwa kuwa Mfalme Mfalme Leopold aliwauwa Wakongo kati ya milioni 10 hadi 15 na mamilioni wengine walibaki na vilema vya maisha, ingawa hakuna mtu anayezungumzia suala hili lakini Mmishonari Mwingereza, Alice Seeley Harris alitumia kamera yake ya sahani kavu aina ya ya Kodak kupata kumbukumbu za ukatili uliofanywa nchini Kongo na serikali ya Ubelgiji.
Kuna taarifa kuwa ukifika Nchini Ubelgiji, kuna majengo ya kihistoria kama Hippodrome Wellington Racetrack, The Maria Hendrickapark, The Royal Museum for Central Africa, The DudenPark na mengineyo, yaliyo maalum kwa historia ya utawala wa Mfalme Leopold ambayo yalijengwa kwa mali zilizochotwa Zaire (DRC).