Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Wilson Charles amewataka Watalaamu wa Afya Mkoani Mwanza, kuimarisha na kuboresha utekelezaji wa mikakati na afua za kudhibiti Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Dkt.Charles, ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani humo, iliyolenga kukagua utekelezaji wa afua mbalimbali za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo, unaoendelea katika Halmashauri za Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela, Magu na Ukerewe.
Katika ziara yake, Naibu Katibu Mkuu huyo amekutana na viongozi mbalimbali wa Mkoa na kushiriki katika kikao cha kamati ya kitaalamu cha sekta zote cha kila siku asubuhi.
Aidha, Dkt.Charles pia alipata taarifa fupi ya mwenendo wa mlipuko na utekelezaji wa afua za udhibiti, na baada ya kupokea taarifa hizo ametoa maelekezo mbalimbali ikiwamo kuimarisha utekelezaji wa afua za kudhibiti ugonjwa huo.