Mkaguzi wa kata ya Mkundi Mkoani Morogoro Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Anna Manumbu amesema kwa kushirikiana Walimu na Wanafunzi, Jeshi la Polisi wataunda club za kupambana na uhalifu mashuleni ambazo zitaongeza kasi ya kupambana na uhalifu na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Manumbu ameyabainisha hayo hivi karibuni na kuongeza kuwa, endapo club za kupambana ana uhalifu mashuleni zikiimarishwa mashuleni zitaibua taarifa nyingi za uhalifu wanaofanyiwa baadhi ya wanafunzi katika kata hiyo.

Amesema, kwa kufanya hivyo itasaidia kuondoa changamoto ya kupata taarifa sahihi pindi changamoto inapotokea ya uhalifu na unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa baadhi ya wanafunzi katika eneo hilo la kata ya Mkundi wilaya Morogoro Mjini Mkoani Morogoro.

Aidha, Manumbu pia amewataka walimu kutengenezea mahusiano mazuri na kubadilishana taarifa kutoka kwa wananfunzi, wazazi na walezi wa wanafunzi hao ili kupata taarifa sahihi pindi wanafunzi hao wanapopata changamoto.

Wataalam wa Afya kuboresha mikakati udhibiti Kipindupindu
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 22, 2024