Zaidi ya Wanafunzi 40 wa Shule ya Sekondari Kingalu iliyopo Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro, wamenusurika kifo baada ya shule hiyo kupigwa na Radi iliyoambatana na mvua kubwa.
Mkuu wa Shule hiyo, Miyango Msilanga amesema Wanafunzi 25 kati yao wamekimbizwa Hospitali ya Rufaa Mkoani humo ili kuendelea kupata matibabu.
Amesema, baada ya tukio hilo baadhi ya Wanafunzi waliopoteza fahamu na walipatiwa huduma ya kwanza shuleni hapo.
Kwa upande wake Afisa Mahusiano Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Morogoro, Beatrice john amethibitisha kupokea wanafunzi hao na amesema kwa sasa bado wanaendelea na matibabu.