Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Sulemani Mwenda amewataka Wafanyabiashara waliopandishaji wa bei ya Sukari kupeleka Risiti za sehemu walizonunulia Sukari, ili awasaidie kurudishiwa fedha zao la sivyo watatozwa faini ya shilingi Milioni 1.5.

Mwenda ametoa agizo hilo mara baada ya kumalizika kwa operesheni ya kuwakagua Wafanyabiashara wanaouza Sukari kwa bei ya shilingi 4,000 badala ya 2,800 Hadi 3,000 kwa kilo kwa bei elekezi iliyotolewa na Serikali Januari 23, 2024 kupitia tangazo Na. 40B.

Operesheni hiyo, iliongozwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya ambayo ilikagua maduka ya wafanya Biashara wa jumla katika mji wa Kiomboi Bomani, Old-kiomboi, Misigiri na shelui na baadhi ya Wafanyabiashara walikiri kuuza Sukari kwa bei ya Tsh 3800 huku wenye maduka madogo madogo ikiuza kwa shilingi 4,000 kwa kilo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora aliwaonya Wafanyabiashara waliopandisha bei tofauti na ile iliyo elekezi kuwa Sheria itafuata mkondo wake na Halmashauri haitakubali Wananchi wake kuibiwa.

Tangazo la Serikali no. 40B aya ya 3(2) na kifungu cha 11A ya 2024 lilielekeza kiwango cha juu cha bei kwa bei ya Sukari ya mauzo ya jumla na rejareja Kanda ya kati inayoundwa na Mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora kuwa ni shilingi 2,650 Hadi 2,800 kwa bei ya jumla na kati ya shilingi 2,800 Hadi 3,000 kwa bei ya rejareja.

Daniel Amartey aikataa Black Stars
Wanafunzi wanusurika kifo kwa radi Morogoro