Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewatahadharisha wale wote wanaojihusisha na uvuvi haramu kuacha vitendo hivyo mara moja, huku akisema atakayekamatwa Serikali itachukua hatua kali dhidi yake.
Waziri Ulega ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano na Wavuvi wa Mwalo wa Magarini, uliopo Wilayani Muleba, Mkoani Kagera.
Amesema, “Wavuvi haramu acheni kazi hiyo mara moja, safari hii tutaifanya oparesheni kisayansi bila kelele, nawatahadharisha mnaofanya vitendo hivyo tutawakata ndani nyumbani kwako bila hata wewe mwenye kujua, tunao uwezo huo, kuweni waungwana, tabia hiyo haivumiliki.”