Wananchi wa Njombe mjini mkoa wa Njombe Wameaswa kuacha tabia kutelekeza kwa kisingizio cha kukosa huduma kutoka kwa wenza wao.
Akitoa elimu kwa Wananchi hao,  Polisi Kata ya Mjimwema Mkaguzi wa Polisi, Alexander Makwasa amesema wananchi wengi wamekuwa na desturi ya kuacha watoto wanahangaika kwa kisingizio hicho.
Amesema, Wananchi hao wanatakiwa kujiunga na vikundi vikundi vidogo ili kupata Mikopo ambayo inaweza kuwasaidia kujikwamua katika hali ngumu ya uchumi.
Aidha, Makwasa pia amewataka Wananchi hao kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na watu wanaojihusisha vitendo vya ukatili.

Mwakinyo: Kuna watu hawanitakii mema
Simba SC yaanza kambi bila Benchikha