Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa siku 30 kwa Mkandarasi Halem Construction kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Maji Navanga unaotekelezwa eneo la Mtama Mkoani Lindi.
Waziri Aweso ameyasema hayo alipofika Jimbo la Mtama kutembelea na kukagua mradi wa Maji ukanda wa Navanga unaotekelezwa katika kata 5 zilizopo katika Wilaya ya Lindi, ambao kwasasa umefikia asilimia 90.
Mradi huo wenye thamani ya Bilion 4.5 utahudumia Vijiji hivi vyenye jumla ya watu 17,015 wenye wastani wa mahitaji ya Maji lita 425,375 kwa siku.
Aidha, Waziri Aweso amefikisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye aliyemuomba kufika Navanga baada ya kuupigania mradi huo unaotarajia kukamilika.