Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi kwa kuteua
Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Waziri mmoja ambapo amemteua aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Soraga kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, akichukua nafasi ya Simai Mohamed Said aliyejiuzulu.

Katika uteuzi huo, Dkt. Mwinyi pia amemteua Ali Suleiman Ameir (Mrembo), kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu ambaye awali alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na kumteuwa Shaaban Ali Othman kuwa Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ambapo awali alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini.

Wengineni Juma Makungu Juma, ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, wakati Salha Mohamed Mwinjuma ameteuliwa kuwa Naibu Waziri
wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, akiachia nafasi yake ya uwakilishi wa Viti Maalum kutoka Kundi la Vijana Kusini, Unguja.

Aidha, Dkt. Mwinyi pia amemteuwa Zawadi Amour Nassor kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini, ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Konde, Mkoa wa Kaskazini, Pemba huku taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said ikieleza kuwa, uteuzi huo unaanza hii leo Januari 27 , 2024 na Viongozi walioteuliwa wataapishwa baadaye.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 28, 2024
Mkandarasi apewa siku 60 kukamilisha mradi wa Maji