Baada ya Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Simai Mohamed Said kudai amemuandikia amemwandikia Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu, huku akilalamikia mazingira yasiyo rafiki katika utekelezaj wa majukumu yake ya kila siku, Serikali ya Zanzibar kupitia kwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi imesema Rais Dkt. Mwinyi ameridhia ombi hilo.

Kupitia taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari, imeeleza kuwa kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 129 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais Dkt. Mwinyi amekubali ombi la kujiuzulu kwa Simai kuanzia Januari 26, 2024.

Simai mwenyewe kupitia Picha mjongeo aliyoisambaza kwenye mtandao wa kijamii, alisema kuwa amemwandikia Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi barua hiyo ya kujiuzulu, akilalamikia mazingira yasiyo rafiki katika utekelezaj wa majukumu yake.

Alisema, “Nimefikia uamuzi huu ambao ni mgumu kwa utamaduni kwa Kizanzibari, kutokana na imani yangu kuwa jukumu namba moja la wasaidizi wa Rais, wakiwemo mawaziri ni kumsaidia katika kutekeleza ilani ya chama tawala na ikitokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi.”

Aidha Simai aliongeza kuwa, “ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni,” amebainisha Simai, ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Tunguu kupitia CCM.”

Aliteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Mambo Kale mwezi Machi mwaka 2022, akitokea katika nafasi ya Naibu waziri wa Elimu aliyoipata mwaka 2019 na siku chache zilizopita, alidai kusikitishwa na maamuzi ya Bodi ya vileo Zanzibar, iliyosababisha upungufu mkubwa wa bidhaa hizo kwenye hoteli za kitali visiwani humo.

Kwa mujibu wa Simai, alisema maamuzi ya bodi hiyo ya kuwabadilisha wasambazaji wa vileo kutoka Tanzania bara na nje ya nchi, bila kuwashirikisha wadau wa utalii visiwani humo, kuliathiri uendeshaji wa sekta hiyo.

AFCON 2023 yamng’oa Djamel Belmadi
Real Madrid kinara wa mapato duniani