Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, limefanikiwa kukamata gari dogola kusafiria aina ya Noah, likiwa linasafirisha na magunia kumi ya dawa za Kulevya aina ya Bangi.
Gari hiyo yenye namba za usajili T777 CBC imekamatwa na Polisi katika eneo la Kijiji cha Chamgata, kilichopo Kata ya Kalemela Wilayani Busega mkoani Simiyu.
Dereva wa gari hilo, alitelekeza gari hiyo pembezoni mwa barabara ya Mwanza kuelekea Musoma na kutokomea kusikojulikana na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.