Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Angola, Jacinto Dala, amesema walistahili kufuzu Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’, inayoendelea nchini lvory Coast.

Angola maarufu kama ‘Swala Weusi’ hawakuzuilika dhidi ya Namibia walipowalaza mabao 3-0, huku Jacinto Dala akihusika katika mabao yote matatu.

Mshambuliaji huyo aliishia kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kwa kiwango chake bora, ambapo ni mara ya pili anaitwa kwenye michuano hiyo.

Dala alipongeza kiwango cha wachezaji wenzake na kuashiria kuwa walistahili kufuzu Robo Fainali hiyo.

“Tulikuwa na uchezaji mzuri sana dhidi ya Namibia. Timu hii ilistahili kufuzu na nina furaha sana tulifanya hivyo.

Nitasema kujitolea na ushiriki wa wachezaji wote ulinisaidia kushinda mchezaji bora wa mechi,” alisema.

Mabao hayo mawili yanamaanisha kuwa Jacinto Dala sasa amefunga manne kwenye michuano hiyo na sasa amepitwa bao moja tu na Emilio Nsue wa Equatorial Guinea mwenye mabao matano.

“Kufunga mabao hapa kunanifurahisha na ningependa kuendelea kufunga katika mashindano haya na kupata ushindi pia,” aliongeza.

Mradi mpango wa Mattei kuinufaisha Tanzania
Mbinu za uhalifu zazidi kugonga mwamba