Ukiwaona kwa mbali unawea kufikiri ni Washehereshaji wa ngoma za kiasili kutoka kabila fulani la Taifa la Marekani ama Uingereza au kutoka eneo lolote Duniani lakini sio Afrika.

Watu hawa, kama utabahatika kuongea nao wanaweza kukupa hata simulizi za Dunia nzima huku wakijinasibu kuwa wanaweza kutibu, kuvaa vibaya na zaidi watakupa hadithi za kutisha.

Muonekao wao, aina ya mavazi yao na hata rangi zao ukiwaona waweza usipate jibu wanatoka wapi lakini uhalisia ni kwamba asili yao ni kutoka Scotland na Ireland.

Wana kigoma chao wanakiita ‘Halloween’ hili ni neno la kale la Kiskoti linalotumika kwa sikukuu zote za Hallows, siku takatifu yenye asili iitwayo Samhain ya kipagani.

Siku ya tukio, huvalia vinyago vya kutisha na mavazi ya kutisha wakidai eti wanawatisha pepo wabaya, halafu mwishoni mwa sherehe huonesha ishara kupitia vinyago walivyovaa wakidai kitendo hicho pia humtisha shetani. “Ama kweli Duniani kuna mambo nyie.”

Ahmed Mussa apata majanga Ivory Coast
Onuachu: Tusiichukulie poa Angola