Ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said kutangaza kujiuzulu nafasi yake akisema mazingira ya kutekeleza jukumu hilo yamekuwa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Mawaziri wanaojiuzulu kuwa wakweli na si kuwaaminisha Watu kinyume chake.

Rais Mwinyi ameyasema hayo hii leo Februari 1, 2024 katika hafla ya kuwaapisha Mawaziri wapya Ikulu Zanzibar na kuongeza kuwa Uwaziri siyo nafasi ambayo mtu atakaa nayo maisha yake yote, kwani kuna njia nyingi ambazo zitakutoa kwenye Uwaziri, aidha utaondolewa au utawajibika kwa tatizo litakalotokea.

Rais Dkt. Mwinyi akipata kumbukumbu ya Picha wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri wapya aliowateua hivi karibuni viwanja vya Ikulu Zanzibar hii leo Februari 1, 2024.

Amesema, “Serikali inapoa amua jambo na wewe hukubaliani nalo, unatoka unajiuzulu kwasababu hukubaliani na maamuzi yaliyotolewa na Serikali lakini kuna jambo moja lazima tukumbushane, wakati unawajibika kwa njia yeyote ile ya kwanza au ya pili ni lazima uwe mkweli na ukweli ninaozungumzia hapa ni kama kuna mgongano wa maslahi.”

Aidha, Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa, “unapochukua sekta hizi ujue kuna matatizo yanayoweza kutokea na matatizo hayo wala si lazima usababishe wewe na pale ambapo haukubaliani na Serikali sema na kuwa muwazi tutakuheshimu, kama tumezuia kitu na wewe una biashara hiyo tangaza, sema ukweli, hapa kuna mgongano wa kimaslahi Mimi ni muagizaji wa kitu fulani na nyinyi mmezuia lakini ukitoka halafu ukaenda kuwaamisha Watu kinyume chake si sahihi.”

Dkt. Mwinyi ataka kasi mara mbili kuwatumikia Wananchi
Sinayoko: Mali ina deni AFCON 2023